Magoli mawili ya Thomas Müller sambamba na yale ya Mario Gomez na Arjen Robben yaliipa ushindi mnono Bayern Munich wa magoli manne kwa bila dhidi ya Barcelona ambayo ilikuwa na nyota wake wote wakutegemewa,akiwemo Xavi, Iniesta na Messi ambaye alikosa michezo kadhaa za ligi ili awefiti kwenye mechi ya Bayern. Kichapo cha goli nne kwa bila ni kipigo cha mara ya kwanza kwa Barcelona kukipata tangu mwaka 1997 walipofungwa na Dynamo Kiev ya Urusi kwenye hatua ya robo fainali kwenye michuano ya UEFA champions. Bayern Munich ambao wameshatangazwa mabingwa wa Ujerumani wiki chache zilizopita kama watafanikiwa kutinga fainali itakuwa ni fainali yao ya tatu mfululizo kushiriki ndani ya miaka minne. Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes awali alisema haogopeshwi na urejeo wa Lionel Messi,na katika mchezo huo Messi alibanwa vya kutosha na mabeki wa Bayern kiasi kwamba hakuweza kupiga shuti hata moja.
Matokeo haya yanafanya mchezo wa marudiano utakaochezwa wiki ijayo kuwa mgumu kwa Barcelona kwani haijawahi kutokea timu kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kufungwa magoli manne na zaidi katika mchezo wa kwanza kisha kuyarejesha katika mchezo wa marudiano na kufuzu hatua inayofuata. Nao mahasimu wakubwa wa Barcelona, Real Madrid nao walikuwa na kibarua kikubwa mbele ya Borussia Dortmund baada ya kupokea kichapo cha goli nne kwa moja kwenye uwanja wa Signal-Iduna-Park, licha ya kuwa Madrid wao wanatofauti ndogo ya magoli kwani watahitaji ushindi wa goli tatu kwa bila kupita tofauti na Barcelona wanahitaji ushinda wa goli tano kwa bila ili kufuzu.
No comments:
Post a Comment