Chama cha soka nchini Uingereza FA kimemfungia mechi kumi mchezaji wa Liverpool Luis Suarez baada ya kumng'ata beki wa Chelsea Ivanovic. Adhabu hii itamfanya Suarez awe nje ya uwanja hadi mwezi wa tisa mwaka huu katika msimu ujao wa ligi. Liverpool iliyobakiza mechi nne msimu huu itacheza bila Suarez hadi msimu ujao ambapo Suarez atakosa mechi sita za mwanzo. Mbali na adhabu hiyo ya FA, klabu ya Liverpool pia imemwadhibu mchezaji huyo kwa kupiga faini ya paundi 200,000 ambazo ni mshahara wake wa wiki mbili. Luis Suarez amekuwa akihusika na matukio ya utovu wa nidhamu mara kwa mara ikiwemo kumwambia maneno ya kibaguzi beki wa Man utd Patrice Evra mwaka 2011 na mwaka 2010 alifungiwa kucheza mechi saba na chama cha soka nchini Uholanzi baada ya kumng'ata beki wa PSV Bakkal
No comments:
Post a Comment