Kipa wa QPR Julio Cesar ameomba msamaha kwa klabu yake na wapenzi wa QPR baada ya kuvaa jezi ya Chelsea kwenye birthday party ya David Luiz. Luiz ambaye ni mchezaji wa Chelsea alifanya party ya birthday yake kwa kufikisha miaka 26 na alimwalika rafiki yake wa karibu Cesar katika party hiyo jambo ambalo lilimfanya avae jezi ya Chelsea kumpa kampani rafiki yake, lakini kitendo hicho kiliwachukiza mashabiki wa QPR na kumuomba Cesar aombe radhi. Cesar kwa kutambua kosa hilo aliomba radhi kwa uongozi wa QPR pamoja na mashabaki kwa kitendo cha kuvaa jezi ya Chelsea ikiwa yeye ni mchezaji wa QPR.
Julio Cesar kulia akiwa pamoja na Luiz na familia yake katika party |
No comments:
Post a Comment