Tuesday, April 30, 2013

Real Madrid wametolewa kiume kwa magoli 3-4 BVB

Timu ya Real Madrid imetolewa kwenye michuano ya UEFA champions na Dortmund baada ya ushindi wa magoli finyu 2-0 hivyo kuiwezesha Dortmund kusonga mbele na kuingia fainali kwa jumla wa magoli 4-3. Real Madrid ilicheza mchezo mzuri wa kuvutia na kwa kasi kubwa tokea mwanzo hadi mwisho wa mchezo lakini safu yake ya ushambuliaji haikuwa makini kumalizia mipira ya mwisho. Cristiano Ronaldo, Higuain, Ozil, Kaka na Di Maria wamechezea nafasi nyingi sana ambazo kama wangezitumia vizuri basi Real Madrid wangeweza kutoka kifua mbele kwa magoli mengi. Golikipa wa Dortmund pia alionesha umahiri wake mkubwa sana baada ya kuokoa mipira mingi ambayo ilikuwa ni magoli ya wazi. Katika mahojiano kabla ya mechi Jose Mourinho kocha wa Real Madrid alisema watakwenda kupigana kufa na kupona na kucheza kwenye kiwango chao cha juu kuliko siku zote, ni kweli wachezaji wa Real wametekeleza aliyosema Jose lakini umahiri wa mabeki wa Dortmund ndiyo umeifanya timu hiyo iweze kuhimili mikiki ya Real Madrid. Hivyo hadi mwisho wa mchezo Real Madrid 3-4 Dortmund. Mchezo mwingine wa nusu fainali utachezwa leo usiku jumatano kati ya Barcelona na Bayern Munich, ikiwa pia ni mchezo wa "mission impossible" kwa Barcelona kwani watahitajika kuwafunga Bayern magoli matano kwa bila ili wafuzu jambo ambalo matokeo yake yanawezekana kimahesabu kuliko kiuhalisia. Magoli yalifungwa na Benzema 83, Sergio Ramos 89. 

Vikosi vya timu zote mbili

Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Ramos, Varane, Coentrao (Kaka 57); Xabi Alonso (Khedira 67), Modric; Di María, Özil, Cristiano Ronaldo, Higuaín (Benzema 57)

Borussia Dortmund: Weidenfeller; Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer; Bender (Santana 90), Gundogan; Gotze (Grosskreutz 14), Reus, Blaszczykowski; Lewandowski (Kehl 87)

Is it on? Sergio Ramos makes it 2-0 and gives Madrid hope
Benzema na Ramos wakishangilia goli la kwanza la Real Madrid lililogungwa na Benzema dakika ya 83
Wrestle for the ball: Real Madrid players fight with Dortmund's goalkeeper Roman Weidenfeller after the first goal
Ronaldo, Benzema na Ozil wakigombania mpira dhidi ya goli kipa wa Dortmund baada ya goli la kwanza kufungwa, golikipa wa Dortmund aling'ang'ania mpira ili kupoteza muda
Down and out: Ronaldo gestures after being knocked to the floor
Ronaldo akinyoosha mikono kuomba penati baada ya kuangushwa katika dakika ya 92 ya mchezo, lakini refa hakutoa penati kwasababu aliangushwa hakiwa bila mpira
No way Jose: Mourinho shows his frustration on the sidelines
Mourinho akishangaa pia kufuatia kitendo cha refa kugomea penati baada ya Ronaldo kuangushwa chini dakika ya 92
End of the road: Ronaldo walks on the pitch looking dejected
Cristiano Ronaldo akitoka nje wa uwanja kwa masikitiko baada ya mchezo kumalizika kwa matokeo ya jumla Real Madrid 3-4 Dortmund
HANDBAGS ... Sergio Ramos has a friendly word with Robert Lewandowski
Vita ilikuwa kali kati ya Ramos na Lewandowski, katika mchezo uliopita Jose Mourinho alisema mabeki wake hawamkufanyia rafu za kutosha Lewandowski ndiyo maana aliwafunga magoli mengi, akasema mchezo wa marudiano vijana wake watamchezea rafu za kutosha Lewandowski kitu ambacho walikitekeleza, ikiwemo kumpiga viwiko, kumkanyaga na kumsukuma

No comments:

Post a Comment