Saturday, July 27, 2013

Klabu ya Liverpool kuuzwa baada ya kuingia hasara

Liverpool
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari nchini Uingereza zinasema mmliki wa klabu ya Liverpool anatarajia kuiweka sokoni klabu hii baada ya kula hasara tokea ainunue miaka mitatu iliyopita. The Sun linaripoti kuwa mmlikini wa Liverpool John Henry aliinunua klabu hii kwa paundi mil 300 mwaka 2010 na hadi sasa ameshatumia jumla ya paundi mil 187 kununua wachezaji lakini wachezaji hao hawajaweza kuleta matunda ya aina yoyote. Mmliki huyo alitolea mfano wa hasara kubwa aliyoingia ni Andy Carroll mchezaji aliyenunuliwa kutoka Newcastle kwa paundi mil 35 na kucheza msimu mmoja tu na baadaye kuuzwa West Ham kwa paundi 19 million. Kwa upande wa Luis Suarez, mmliki huyo alisema anafurahi kuwa kuuzwa kwake kutaingiza pesa nyingi, lakini alisikitishwa na utovu wake wa nidhamu ambao umeigharimu sana klabu. 'Suarez ameharibu jina la klabu na pia kukosekana kwake kwenye mechi muhimu za ligi kumefanya tupate matokeo mabaya'.

Klabu ya Liverpool imekuwa ikifanya vibaya kwa miaka ya karibuni tofauti na ilivyokuwa. Kiwango cha Liverpool kilikuwa ni kushindania ubingwa wa ligi na klabu bingwa Ulaya, lakini kwasasa klabu ya Liverpool ina muda hajafanikiwa kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya na imekuwa kawaida kumaliza ligi kwenye nafasi ya tano au sita. 
Kufuatia hali hii, John Henry ameona ni heri kuiuza kuliko kuendelea kula hasara na tayari ameshaanza mazungumzo na kampuni ya mafuta ya Saudi Arabia ijulikanayo kwa jina la Saudi Aramco na pindi watakapokubaliana, klabu ya Liverpool itanunuliwa na matajiri hao wa mafuta. 
John Henry Liverpool owner
John Henry mmliki wa Liverpool wa sasa ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Fenway Sports Group. 

No comments:

Post a Comment