Wednesday, March 27, 2013

Van Persie apiga la 33, amzidi Cruyff


Robin Van Persie mshambuliaji wa Man utd na Netherlands jana alifunga magoli mawili kwa timu  yake ya taifa na kumfanya afikishe jumla ya magoli 33 akimzidi mkongwe Johan Cruyff. Van Persie miaka 29 ameshacheza mechi 74 kwa timu yake ya taifa wakati Cruyff alicheza mechi 48 na kufunga magoli 32. Katika historia ya soka nchini Netherlands, Cruyff ni mchezaji ambaye anakumbukwa hadi leo na amekuwa mfano kwa Waholanzi. Cruyff alikuwa na rekodi ya kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mara tatu mfululizo rekodi ambayo imevunjwa na Lionel Messi mwaka jana baada ya kushinda mara ya nne. Cruyff aliacha kucheza soka mwaka 1984 na ndiye alikuwa mpinzani mkubwa wa Franz Beckenbauer na Gerd Muller kama ilivyo Messi na Ronaldo kipindi cha sasa. Hivyo Robin Van Persie ameandika historia ya peke kumzidi mkongwe Cruyff katika historia ya magoli nchini Holland.   

No comments:

Post a Comment