Thursday, March 28, 2013

Huu sio muda wa kupoteza pointi – Wenger

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa huu sio muda wa kupoteza tena pointi. Wenger ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na DailyMail kuhusu nafasi ya Arsenal katika michuano ya UEFA ijayo. Wenger alisema “Matokeo yetu na Bayern Munich na Swansea ni ishara tosha kuwa sasa hivi Arsenal tupo kwenye ‘form’ tutaendelea na mwendo huo huo, tumebakiza mechi tisa, tano nyumbani na nne ugenini , kwa form tuliyonayo nne bora lazima tuwepo”. Najua Theo na Jack hawataweza kucheza mechi za karibuni  lakini hilo halituogopeshi kwani kikosi chetu ni imara ila tunawatarajia watapona baada ya muda mfupi. Hayo yalikuwa ni maneno ya Arsene Wenger, Arsenal ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 50 na mchezo mmoja mkononi chini ya Spurs wenye pointi 54, wikiendi hii Arsenal itakuwa nyumbani ikicheza na Reading.     

No comments:

Post a Comment