Mchezo wa Simba na Azam umekwisha hivi sasa na matokeo ni droo 2-2. Kwa matokeo haya Simba wamejiondolea matumaini ya kushika nafasi ya pili kwani imefikisha pointi 36 na kubakiza mechi nne wakati Azam inayoshika nafasi ya pili wamefikisha pointi 47 na kubakiza mechi tatu. Kama Simba watashinda mechi zote zilibakia watafikisha pointi 48 huku wakiombea Azam FC wapoteze michezo yake yote iliyobakia. Matumaini ya Simba yanategemea muujiza kwani sio rahisi kwa Azam kupoteza michezo yote mitatu iliyobakia. Azam FC wamebakiza pointi mbili tu kuwatoa Simba kwenye mbio za kuwania nafasi ya pili. Pia, kwa matokeo ya leo Azam FC itakuwa imejiweka kwenye nafasi ngumu kuwania ubingwa kwani Yanga wana pointi 52, watahitaji pointi tano tu kujihakikishia ubingwa.
No comments:
Post a Comment