Kuelekea kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA cup, Juan Mata
kiungo wa Chelsea amemfagilia Yaya Toure wa Man city kuwa ni kiungo
aliyekamilika. Mata alisema “ Yaya ni kati ya viungo bora duniani, anaweza kuzuia,
kushambulia na kufunga, ni mchezaji mwenye nguvu na pia mrefu, kwa kweli ana
kipaji cha kipekee sana, tutahitaji nguvu za ziada kumzuia. Chelsea tuna viungo
na mabeki wazuri tutaweza kumzuia licha yakuwa atatusumbua”. Mata aliyasema
hayo alipokuwa akihojiwa na jarida la “The Sun” kufuatia mchezo wa jumapili
ambao ni muhimu sana kwa timu zote Chelsea na Man city ikiwa kila timu
inahitaji ushindi ili iweze kuweka heshima baada ya kukosa kombe la ligi na
UEFA champions.
No comments:
Post a Comment