Bingwa wa mbio fupi duniani Usain Bolt atajumuika pamoja na wachezaji wengine wa Man utd kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sevilla tarehe 9 Agosti. Rio Ferdinand ndiye aliyemshawishi kocha wa Man utd David Moyes kumjumuisha Bolt kwenye kikosi cha mechi hiyo ili kutimiza ndoto za Bolt za kutaka kuchezea Man utd na vilevile, uwepo wa Bolt utahamasisha watu wengi kuhudhuria kwenye hiyo mechi. Bolt ameshatamka mara nyingi nia yake kutaka kucheza Man utd pindi atakapostaafu kukimbia, amesema anataka kutumia mechi hiyo kama majaribio na ushawishi kwa Moyes ili muda ukifika aweze kumsajili. Kufuatia taarifa hizi, wadau wengi wa soka wameanza kuiongelea mechi hiyo wakilinganisha kasi ya Bolt kwenye riadha na ndani ya dimba la soka. Sijui itakuwaje??. Mechi hii kati ya United na Sevilla itakuwa ni maalumu kwa ajili ya Rio kwa kufikisha miaka 11 akiwa na Man utd. |
Sunday, July 7, 2013
Bolt kucheza kwenye kikosi cha Man utd vs Sevilla
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment