Friday, April 19, 2013

Makocha wa Azam FC na AS FAR watambiana

Makocha wasaidizi wa timu zote mbili Azam FC na AS FAR wametambiana leo katika press conference juu ya mechi yao itakayofanyika April 20 uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Kalimangonga Ongala wa Azam FC alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu mechi hiyo, alisema wamejiandaa vya kutosha na wanaahidi Watanzania kuwa wataibuka na ushindi mnono. Ongala pia alisema katika maandalizi yao walifanikiwa kupata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wamezifanyia kazi. Naye Ouadani wa AS FAR amesema hawaifahamu vizuri Azam FC, lakini wanaujua mpira wa Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jijini Dar es Salaam Machi 24 mwaka huu na Stars kushinda mabao 3-1, kocha huyo amesema kupitia mechi hiyo ya Tanzania wameweza kujifunza kidogo mtindo wa uchezaji mpira wa Tanzania kitu ambacho anasema kitawasaidia. 
Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi ndani ya uwanja wa Azam Chamanzi jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wao dhidi ya AS FAR
Azam FC na AS FAR ni timu zenye wachezaji wazuri ambao wanachezea timu za taifa, wachezaji wa Azam FC waliopo kwenye timu ya taifa ambao pia wanatarajia kuwepo kwenye mechi ni pamoja na Aishi Manula, Mwadini Ally, Khamis Mcha, John Bocco na Salum Abubakar wakati AS FAR Rabat ina wachezaji sita kwenye timu ya Taifa ya Morocco ambao mabeki Younes Bellakhdar, Abderrahim Achchakir, Younnes Hammal, na viungo Salaheddine Said, Salaheddine Aqqal na Youssef Kaddioui. Watanzania wanaombwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia Azam FC
Photo: Timu ya AS FAR Rabat ya Morocco imewasili leo mchana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza na Azam FC kwenye mechi ya kombe la Shirikisho Afrika itakayochezwa siku ya Jumamosi 20/4/2013, Uwanja wa Taifa
(Pichani baadhi ya wachezaji wakiwasili Uwanja wa kimataifa wa  Ndege wa Mwalimu Nyerere Dar)
Kikosi cha AS FAR kilipokuwa kikiwasili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambao wamefikia kwenye hotel ya Saphirre Kariakoo. 

No comments:

Post a Comment