Monday, April 8, 2013

Villas Boas ameanza kukata tamaa


Kocha wa Tottenham Villas Boas ameonesha kuanza kukata tamaa ya kucheza champions league msimu ujao baada ya kutoka droo ya goli 2 kwa 2 dhidi ya Everton. Villas Boas ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na ESPN na kukiri kuwa Tottenham imebakiza mechi ngumu kuliko wapinzani wao Arsenal. Villas Boas alisema “sisi tuna mechi mbili ngumu dhidi ya Chelsea na Man city, hizi mechi mbili ndiyo zitatoa matokeo ya mwisho kama tutafuzu kushiriki UEFA champions, lakini wenzetu Arsenal wamebakiza mchezo mgumu mmoja tu dhidi ya Man utd mchezo ambao hauna ushindani kwasababu Man utd wameshajua wao ni mabingwa, hivyo mechi zetu ni ngumu kuliko za Arsenal zilizobakia”. Tottenham kwasasa wana pointi 58 wakati Arsenal wana pointi 56 wakiwa na mchezo mmoja mkononi. 

No comments:

Post a Comment