Sunday, April 7, 2013

Mechi ya Azam yaingiza mil 44.2


Mechi kati ya Azam ya Tanzania na Barrack Young Controllers II ya Liberia iliyochezwa jana Aprili 6 imeingiza sh. 44,229,000. Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana. Katika mchezo huo watazamaji waliokata tiketi walikuwa 17,128. Viingilio vilikuwa sh. 2,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Kiingilio cha sh. 2,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 15,212. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 5,798,025, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 3,865,350 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 28,990,500.

No comments:

Post a Comment