Sunday, April 7, 2013

Vucinic hana aibu

Vucinic akivua bukta
Mshambuliaji wa Juventus Mirko Vucinic jana (6/4/13) alivua bukta baada ya kufunga goli dhidi ya Pescara katika mchezo wa ligi kuu ya Italia. Vucinic alipohojiwa kwanini alifanya kitendo hicho alisema “nilijikuta navua tu bukta, haikuwa ni jambo la kujifikiria, nilijisikia nikavua". Katika tukio hilo refa alimpa kadi ya njano Vucinic adhabu ambayo ni sawasawa na ile anayopewa mchezaji aliyevua shati jambo ambalo FIFA inatakiwa iliangalia upya ili adhabu ya kuvua bukta iwe kali kuliko kuvua shati. Katika mchezo huo Juventus ilishinda kwa goli 2-1 na imeweza kufikisha pointi 71 ikiwa bado nafasi ya kwanza na tofauti ya pointi 12 dhidi ya Napoli inayoshika nafasi ya pili yenye pointi 59. 

Vucinic akishangilia akiwa amevua bukta yake

No comments:

Post a Comment