Klabu tajiri ya PSG imetangaza rasmi nia yake ya kuwanunua Rooney na Nani wa Man utd kwa jumla ya paundi milioni 40. Akiongea kwenye French TV mshauri mkuu wa PSG bwana Michel Moulin amesema mpango wa kuwanunua Rooney na Nani umeshakalika na wachezaji hawa wanatarajiwa kuwasili jijini Paris mwishoni mwa msimu kwa ajili ya vipimo na kufunga mkataba. Sir Alex amekuwa akiwaweka benchi Rooney na Nani mara kwa mara na swala hili limehusishwa na mipango huo wa kuhamia PSG. PSG tokeo inunuliwe na Qatar Investment Authority imekuwa kwenye kipindi cha kujiboresha kwa nunua wachezaji wenye uwezo zaidi ili kuleta ushindani kwenye ligi ya ndani na michuano ya kimataifa, hadi sasa PSG imeweza kuwasajili Ibrahimovic, Beckham, Pastore, Silva, Motta na Alex. Mafanikio ya PSG yameshaanza kuonekana baada ya kufanikiwa kushiriki UEFA mwaka huu na kufikia hatua ya robo fainali kabla ya kutolewa kwa tabu na Barcelona kwa goli la ugenini.
No comments:
Post a Comment