Torres, Terry na Lampard wakiwa benchi dhidi ya Man city |
Beki mkongwe wa Chelsea John Terry ameikana kauli ya kocha
wake Rafa Benitez kuwa yeye hawezi kucheza mechi mbili kwa wiki. Terry ameyasema
hayo baada ya Benitez kusema kuwa Terry asingeweza kucheza kwenye mechi dhidi
ya Man city kwasababu alikuwa mgonjwa na hali yake haimruhusu kucheza mechi
zaidi ya mbili kwa wiki. Akimjibu kocha wake John Terry alisema “mimi
nimeshapona naweza kucheza mehi zaidi ya mbili kwa wiki, maneno aliyosema kocha
sio ya kweli”. Benitez na Terry wamekuwa kwenye mgogoro kwa muda mrefu sasa
tokea mwezi wa pili baada ya Chelsea kufungwa na Man city katika mchezo wa ligi
kuu, mgogoro wao ulisababishwa na mfumo mpya aliouleta Benitez ambao Terry
alitofautiana nao. Tesisi zinasema Benitez anatumia kigezo cha Terry kuwa
mgonjwa ili asicheze ila kiukweli bifu lao ndiyo chanzo cha Terry kukaa benchi, vilevile, Frank Lampard pia anahusishwa na bifu la chini chini dhidi ya Benitez mambo ambayo yanamponza Benitez nakumfanya ampoteze mechi ambazo angeweza kushinda.
No comments:
Post a Comment