Mshambuliaji wa Man utd Javier Hernandez baada ya kukaa
kimya kwa muda mrefu amejitokeza wikiendi hii na kusema yeye atapigana hadi
arudishwe kwenye kikosi cha kwanza hata kama Falcao na Lewandowski watasajiliwa
na United. Hernandez ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Dailymail baada ya
fununu kuwepo kwamba Man utd italipa keshi paundi milioni 48 pamoja na
Hernandez juu kwa klabu ya Atletico Madrid ili kumnunua Falcao. Alipouliza
kuhusu hilo Hernandez alisema "hiyo ni mipango ya klabu, ila mimi nitapigana
nibakie Man utd hata kama United italeta mshambuliji mwingine, wachezaji wengi
wanapenda kuwepo United, mimi nimepata nafasi hii lazima niitumie vizuri, hivyo
nitaendelea kuwa mnyenyekevu na kuheshimu maamuzi ya kocha wangu kila siku”.
Hernandez (24) yupo kwenye wakati mgumu kurudi
kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushindani mkali kutoka kwa Van
Persie, Rooney na Welbeck. Hadi sasa Hernandez ameshacheza mechi 15 kati ya
mechi 31 za ligi na amefunga magoli nane hadi sasa.
No comments:
Post a Comment