Monday, April 8, 2013

TFF, wagombea wangojee wajumbe wa FIFA


TFF imesema wagombea wote wenye malalamiko juu ya uchaguzi mkuu wa TFF wangojee ujumbe wa FIFA ili kuwasilisha malalamiko yao lakini sio kuyaongelea kwenye vyombo vya habari. TFF imesema hakuna maana yoyote ya kuongelea maswala hayo kwenye vyombo vya habari kwani wajumbe wa FIFA ndiyo waamuzi wa maswala hayo na wanatarajiwa kuja hivi karibu kusikiliza na kutolea maamuzi mgogoro huo. Wajumbe hao wa FIFA wanakuja nchini baada ya uchaguzi mkuu wa TFF kushindwa kufanyika kufuatia migogoro iliyojitokeza katika hatua za mchujo wa wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa TFF. 

No comments:

Post a Comment