Friday, April 5, 2013

Tottenham maji mazito, majeruhi sita


Club ya Tottenham ipo kwenye wakati mgumu kutetea nafasi yake ya ushiriki wa ligi ya mabingwa barani ulaya kufuatia idadi kubwa ya majeruhi iliyonayo, hadi sasa Tottenham ina majeruhi sita ambao ni Bale, Lenon, Gallas, Sandro, Kaboul na Defoe wachezaji hawa wote wanacheza kikosi cha kwanza na wikiendi hii Tottenham watakutana na Evarton. Mechi hiyo itakuwa ni ngumu kwa Tottenham kutokana na majeruhi waliokuwa nao, zaidi pia Evarton ni timu nzuri yenye ushidani. 
Villas Boas akimwangalia Bale baada ya kuumia kwenye mechi na Basle
Tottenham lazima apigane kufa na kupona katika mechi ya jumapili ili iweze kuendelea kujiweka mbali na Arsenal. Tottenham kwasasa ina pointi 57 na imecheza mechi 31, wakati wapinzani wao Arsenal wana pointi 53, michezo 30 na Chelsea wana pointi 55 na michezo 30. 

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger mapema wiki iliyopita alisema timu yake lazima imalize ligi kwenye nafasi ya tatu au ya nne na wamejipanga kushinda michezo yote iliyobakia. Benitez naye kocha wa Chelsea alisema kwasasa Chelsea hawana pointi za kupoteza. Hivyo timu zote hizi tatu zipo kwenye ushandi mkali sana kuwania nafasi mbili za juu. Wikiendi hii Tottenham atacheza na Evarton, Arsenal atakuwa ugenini kucheza na West Bro, wakati Chelsea atakuwa nyumbani kucheza na Sunderland. 

No comments:

Post a Comment