Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy amesema klabu yake imeanza kuongea na Bale ili kumuongezea tena mshahara kwa lengo la kumshawishi akubali kubaki kwenye klabu hiyo kwa msimu ujao. Levy amesema ' tunatambua mshahara tunaompa Bale haulingani na thamani yake ya sasa, tutajitahidi kuongea naye ili tuweze kumpa mshahara anatakao ridhika'. Bale kwa sasa analipwa paundi 150,000 kwa wiki baada ya kuongezewa mwezi wa tano mwaka huu, wakati Madrid imeahidi kumlipa paundi 200,000 kwa wiki na marupurupu mengine juu. Tayari Rais wa Madrid Perez ameshatoa ahadi ya kumsajili Bale kwa mashabiki wa klabu hiyo, hivyo klabu ya Madrid kwa sasa ipo tayari kulipa kiasi chochote cha pesa. Taarifa kutoka gazeti la Marca zinasema, Bale na Madrid wameshakubaliana na tayari Madrid wameshaanza kuongea na Tottenham ili kumsajili mchezaji huyu, licha ya kuwa, kocha wa Tottenham AVB bado anamng'ang'ania Bale. Historia inaonesha klabu ya Madrid bado haijawahi kumhitaji mchezaji ikashindwa kumsajili, kama itashindikana kumsajili Bale mwaka huu, basi itakuwa ni mara ya kwanza kwa Madrid kushindwa kumsajili mchezaji inayomtaka. |
Thursday, July 25, 2013
Spurs kuongeza tena mshahara wa Bale ili abakie
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment