Monday, May 13, 2013

Arsenal kulipwa paundi mil 3 na Barcelona

Klabu ya Arsenal inatarajia kulipwa paundi mil 3 na Barcelona mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni moja ya makubaliano kwenye mkataba wa kumsajili Fabregas na Alex Song. Barcelona iliwasajili Fabregas na Song mwaka 2011 na 2012 na moja ya makubaliano kwenye mkataba huo ni kwamba ,kama Barcelona itafanikiwa kushinda ubingwa wa ligi italipa paundi mil 3 kwa Arsenal ikiwa ni sehemu ya faida iliyopata kutokana na wachezaji hao. Cesc Fabregas alisajiliwa na Barcelona akitokea Arsenal kwa paundi mil 35 na makubaliano yalikuwa kwamba, Cesc atailipa Arsenal paundi laki 8.8 kila mwaka kwa miaka mitano kutoka kwenye mshahara wake na vilevile Barcelona itailipa Arsenal paundi mil 4.4 kama Barcelona itashinda makombe mawili ya ligi na moja la UEFA champions kwa kipindi cha miaka mitano. Cesc alifanya uamuzi huo wa kulipa mwenyewe sehemu ya ada ya uhamisho kutokana na mapenzi yake ya kutaka kurudi nyumbani licha ya kuwa hadi sasa bado anangojea Xavi astaafu ili aweze kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona. 

No comments:

Post a Comment