Friday, May 17, 2013

Barcelona wahaha kutafuta mbadala wa Messi

Baadaya ya Messi kuonekana ndiyo tegemeo kubwa kwa Barcelona kwamba bila yeye timu inasuasua, uongozi wa Barcelona upo kwenye harakati za kuhakikisha Neymar anasajiliwa kabla ya msimu ujao kuanza. Uongozi mzima wa klabu ya Barcelona akiwemo raisi Sandro Rosell wameshafika nchini Brazil kufanikisha uhamisho wa Neymar. Katika maongezi ya awali klabu ya Santos pamoja na Barcelona walishakubaliana kuwa mchezaji huyo atajiunga na Barcelona baada ya kombe la dunia mwaka 2014, lakini maendeleo mabaya ya Barcelona msimu huu yameufanya uongozi wa Barcelona kuona mwaka 2014 ni mbali sana, hivyo wameamua kupeleka maombi tena kwa klabu ya Santos ili imuachie Neymar mwishoni mwa msimu huu. Maombi hayo ya Barca yameonesha mafanikio kwani Santos na Neymar wameshakubali kwa ada ya Euro 57 mil, lakini kipingamizi kikubwa hadi sasa ni baba mzazi wa Neymar ambaye hataki mtoto wake aondoke kabla ya kombe la dunia. Uongozi wa Barca pamoja na Santos umesema wanaamini wataweza kufanikisha mipango ya uhamisho ndani ya wiki hii na muda wowote wiki hii au wiki ijayo watatangaza rasmi baada ya kukubaliana na baba mzazi wa Neymar. 

Klabu ya Barcelona imefikia hali hii baada ya kufanya vibaya kwenye michuano ya UEFA lakini vilevile wapinzani wao wakubwa Real Madrid msimu huu wameweza kuwafunga mfululizo kitu ambacho imekuwa ni aibu kubwa. Haya yote yametokana na utegemezi waliojiwekea wachezaji wa Barcelona kwa Lionel Messi kiasi kwamba timu haiwezi kucheza vizuri bila Messi na kama Messi akikabwa vizuri asionekane basi safu nzima ya ushambuliaji inaathirika, hali hii imeonekana kwenye mechi za Barcelona dhidi ya Real Madrid, AC milan na Bayern Munich. Katika kulitambua hili uongozi wa Barcelona umeamua kufanya jitihada za kutatua tatizo hili ikizingatiwa pia Messi amepata majeraha ya paja la kulia mwishoni mwa msimu huu, majeraha ambayo haijajulikana kama yataweza kupona mapema na kumuwezesha kucheza kwenye kiwango chake msimu mzima unaokuja. Kama uhamisho wa Neymar ukikamilika mtihani utahamia kwa kocha wa Barca Villanova kuipanga vyema safu yake ya ushambuliaji kwani atakuwa na Neymar, Messi, Iniesta, Fabregas, Alexis, Pedro na Villa, wachezaji wote hawa watataka kucheza.  

Haya ni magazeti mbalimbali ya nchini Hispania ambayo yameshaanza kuandika kuwa Neymar tayari amehamia Barcelona.
mundodeportivo.750  sport.750

No comments:

Post a Comment