Friday, May 17, 2013

Matatizo ya tiketi pambano la Simba vs Yanga

Wapenzi wengi wa soka wamelalamika kuhusiana na uhaba wa tiketi za mpambano wa Simba na Yanga, ambapo tokea jana sehemu nyingi zilikuwa zimeanza kuuza tiketi misululu mirefu ya watu ilikuwepo ili kujipatia tiketi za mpambano huo lakini cha kushangaza tiketi za shilingi 5000 na 7000 zilikuwa zimekwisha kwenye vituo vingi vya kuuzia tiketi na badala yake walionekana baadhi ya watu wasiokuwa rasmi wakiziuza tiketi hizo kwa kwa bei ya juu zaidi. Tiketi za shilingi 5000 zilikuwa zinauzwa 7000 na za shilingi 7000 zilikuwa zinauzwa shilingi 9000. Tatizo hili limepelekea baadhi ya watu kuuziwa tiketi feki kwasababu ya mfumo duni uliotumika kuuzia tiketi kwenye pambano kubwa kama hili ambalo maelfu ya wapenda soka nchini wangependa kwenda kiwanjani kushuhudia. Kutokana na hali hii washabiki wa soka wanaombwa kuwa makini waponunua tiketi vilevile kwa wale wenye subira ni vyema wakaenda uwanjani leo kununulia tiketi mlangoni. 

No comments:

Post a Comment