Baada ya Sir Alex kutangaza kustaafu vyombo vya habari vya
nchini Uingereza vimerioti kuwa David Moyes kocha wa Everton anatarajiwa
kutangazwa kama kocha mpya wa Man utd wiki hii. Uhakika wa kuwa moyes atachukua
nafasi ya Sir Alex bado haujathibishwa na uongozi wa Man utd lakini kocha huyo
alionekana leo mchana kukutana na viongozi wa Man utd kwa maongezi. Moyes
anayefundisha Everton kwa sasa amepewa nafasi kubwa ya kujiunga na United
kutokana na uwezo wake lakini zaidi ni kudumu kwake Everton kwa muda mrefu
tokea mwaka 2002 hadi sasa ikiwa ni mwaka wake wa 11. Tetesi hizi zimezuka baada ya mmoja kati ya viongozi wa juu wa Man utd kusema kocha ambaye ataziba
pengo la Sir Alex ameshapatikana na wanachomalizia kwasasa ni kukubaliana kuhusu
mshahara na maswala mengine ya kiufundi, ila kigogo huyo wa juu alisema kocha
huyo sio Jose Mourinho kama wengine walivyofikiria.
Moyes akiwa ndani ya gari akiendeshwa na wakala wake tofauti na siku za kawaida ambapo huwa anaendesha gari mwenyewe. |
No comments:
Post a Comment