Friday, May 10, 2013

Federer atolewa Madrid open na Nishikori

Bingwa mara 17 wa grand slam duniani Rodger Federer ametolewa katika michuano ya Madrid open na Mjapani Kei Nishikori kwa seti 6-4, 1-6, 6-3. Nishikoni ambaye anashikilia nafasi ya 17 duniani kwenye tenesi hii ni mara yake ya kwanza kumtoa Federer anayeshikilia nafasi ya pili duniani kwa ubora wa tenesi. Kwa matokeo haya Nishikori amefanikiwa kuingia nusu fainali ambapo atakutana na Pablo Andujar . Wakati huo huo Rafel Nadal ameingia robo fainali baada ya kumpiga Mikhail Youzhny kwa seti mbili mfululizo za 6-2, 6-3 ndani ya saa moja. 

No comments:

Post a Comment