Monday, May 20, 2013

Nkamia na Kamata wachangia wizara ya michezo

Vilabu vinapewa fedha kidogo za milangoni 
Mbunge wa Kondoa Juma Nkamia akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya utamaduni, habari, michezo na vijana ameliongelea swala la mgawanyo wa mapato ya mlangoni kwa vilabu vya soka nchini. Nkamia aliyasema hayo kufutia mgao wa shilingi mil 123 kati ya shilingi mil 500 zilizopatikana katika mechi kati ya Simba na Yanga. Akichangia bajeti hiyo Nkamia alisema " Imefikia muda sasa, serikali lazima iingilie kati mgawanyo wa fedha ambazo vilabu vinapewa kwani fedha hizo zimekuwa ni kidogo mnoo, mfano mechi ya jumamosi kati ya Simba na Yanga, timu hizi zimegawana shilingi milioni 246 na kiasi kilichobakia ambacho ni kikubwa cha shilingi milioni 254 zimekwenda kwenye taasisi kitu ambacho sio haki, kwani vilabu husika vinatakiwa kupewa fungu kubwa la fedha kuliko taasisi zinazosimamia michezo". 

Taifa stars ipewe nguvu iweze kushiriki kombe la dunia
Mh. Vicky Kamata  pia katika mchango wake kwenye wizara hiyo aligusia taifa stars pamoja na elimu kwa vijana, Kamata alisema " Wabunge wenzangu, serikali pamoja na Watanzania wenzangu nawaomba tuipe support timu yetu ya taifa (taifa stars), timu yetu imebakiza mechi mbili tu, ikishinda mechi hizo itaingia kwenye hatua ya mwisho kuelekea kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014, naiomba sana serikali iwasaidie vijana hawa kwani wakifanikiwa kuingia kombe la dunia watailetea sifa kubwa nchi yetu. Lakini vilevile napenda kuiomba serikali ifanye kama Korea ya kusini, iwachukue baadhi ya vijana iwapeleke kwenye nchi zilizoendelea wakasomee michezo halafu warudi kufundisha kwenye vyuo vya michezo nchini na vilevile waweze kufundisha timu za Tanzania kuliko kuwategea walimu wa kigeni kila siku".

No comments:

Post a Comment