Wednesday, June 26, 2013

Gerrard yupo fiti, atakuwepo kwenye ziara Asia

Rehab? Steven Gerrard has had a considerable amount of rest
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard anatarajiwa kurudi uwanjani wiki ijayo baada ya kupata nafuu ya majeraha kwenye bega lake la kushoto. Gerrard mwenyewe alithibitisha hayo alipokuwa akiongea na LFC TV akisema ' sijawahi kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kama huu, wiki sita ni nyingi sana, daktari ameniambia nimeshapata nafuu, nina hamu ya kurudi mazoezini kuungana na wenzangu, natarajia kuwepo kwenye safari za Liverpool nje ya nchi kucheza mechi za kirafiki'. Gerrard aliumia bega lake la kushoto mwishoni mwa msimu uliopita, na alifanyiwa upasuaji mdogo ili kurekebisha sehemu iliyoteguka. Majeraha haya yalimfanya akose mechi mbili za mwisho kwenye msimu wa ligi uliokwisha. Klabu ya Liverpool inatarajia kufanya ziara bara la Asia kwenye nchi za Indonesia, Australia na Thailand kuanzia tarehe 20 mwezi Julai. 

No comments:

Post a Comment