Thursday, May 9, 2013

Moyes atangazwa rasmi kuwa kocha wa Man utd

Friends and foes: Moyes was approached by Ferguson as early as 1998
Klabu ya Manchester United imemtangaza rasmi David Moyes kuwa kocha mkuu baada ya Sir Alex kustaafu. Moyes amesaini mkataba wa miaka sita na United lakini ataanza rasmi baada ya msimu huu kuisha. Moyes alipokuwa akihojiwa kuhusiana na jambo hili alikiri kuwa ameshasaini mkataba mpya na United zaidi alisema ' nina furaha kuwa kocha wa klabu kubwa kama Man utd, sijaamini kusikia Sir Alex amenichagua mimi kuchukua nafasi yake, ila nina kazi kubwa ya kuingoza United kwa kudumisha ubora alioutengeneza Sir Alex.  Moyes alijiunga na Everton mwaka 2002 na ameshaiongoza Everton kucheza michezo 516, kati ya hiyo Evertoni ilishinda 217, ilitoka droo michezo 139  na kufungwa michezo 160.  

No comments:

Post a Comment