Sunday, May 26, 2013

Neymar ajiunga rasmi na Barcelona

Hatimaye klabu ya Barcelona imefikia makubaliano na mchezaji wa Santos Neymar kwa mkataba wa miaka mitano. Taarifa hizi zimetangazwa leo asubuhi kwenye mtandao wa Barcelona ukisema “FC Barcelona imeshakamilisha uhamisho na Neymar da Silva Junior”. Neymar ambaye anasemekana kuwa mchezaji mwenye kipaji cha kipekee kwa sasa duniani anatarajiwa kusaini mkataba siku ya jumatatu baada ya kucheza mechi yake ya mwisho na klabu yake jumapili hii itakapokuwa ikicheza na Flamengo. Katika maneno yake Neymar alisema “ imenibidi nitangaze rasmi kuwa nimechagua kwenda Barcelona kabla ya jumatatu haijafika kwasababu kila mtu ameshajua msimamo wangu, nawashukuru sana marafiki, washabiki na wote waliowezesha mafanikio yangu nikiwa na Santos, ninaondoka hapa ila ninamuomba Mungu aniongoze huko nindako”. Neymar amefikia uamuzi wa kujiunga na Barcelona kutokana na mapenzi yake ya muda mrefu ya kupenda kucheza pamoja na Messi, Xavi na Iniesta hivyo malengo yake yameweza kufika na anategemewa kuwa moja kati ya wachezaji muhimu sana ndani ya klabu ya Barcelona misimu ijayo.  

No comments:

Post a Comment