Monday, May 20, 2013

Ngassa asaini rasmi Yanga, ni mchezaji atakayelipwa zaidi ya wote nchini Tanzania

Mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngassa leo amesaini rasmi mkataba mpya na klabu ya Yanga baada ya msimu wa ligi kuu Tanzania bara kuisha. Ngassa aliyejiunga na Simba kwa mkopo akitokea Azam FC, mkataba wake na Azam umekwisha msimu huu. Ngassa mwenyewe amethibitisha hilo baada ya mechi kati ya Simba na Yanga akisema " Nilikuwa kimya kabla ya mchezo huu kwasababu nilikuwa bado natumikia mkataba wangu na Azam ambao umekwisha na sasa nipo huru na ninajiunga na Yanga". Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga utakaomchukua hadi mwaka 2015, mkataba ambao utamfanya Ngassa awe mchezaji anayelipa zaidi ya wachezaji wote Tanzania akiwa anapokea dola 2000 kwa mwezi, Ngassa pia amepewa gari ya aina ya Nissan Xtrial pamoja na tsh mil 10 na Yanga ikiwa ni kama pesa za utangulizi kwani ni mchezaji huru hivyo hakuwa na ada ya uhamisho. 

No comments:

Post a Comment