Monday, May 20, 2013

Matukio ya mwisho wa ligi kuu England

Acrobatic: Koscielny volleys home from inside the box
Case for the defence: Koscielny (right) is mobbed after his goal
Koscielny ndiye aliyekuwa shujaa wa Arsenal baada ya kufunga goli la muhimu kwa timu yake na kuondoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle ushindi ambao umeipatia Arsenal tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya na kuitupilia mbali Tottenham. 
Farewell: Sir Alex Ferguson was given a guard of honour by both teams prior to the match
Goodbye: Ferguson salutes the crowd after his career ends with a 10-goal thriller
Jumapili ya jana pia tulishuhudia Sir Alex Ferguson akifikia ukingoni kuifundisha Man utd kama kocha baada ya kuingoza Man utd kwa kipindi cha miaka 27. Sir Alex alipokelea kwa saluti ya makofi alipokuwa akiingia uwanjani kama ishara ya shukrani na kumuaga akiwa ni moja kati ya makocha wenye heshima kubwa nchini Uingereza na duniani kwa ujumla kwa umaarufu na umahiri wake alioweza kuuonesha kwa Man utd.  
Last hurrah: Paul Scholes comes on as a substitute in his last game before retirement
Paul Scholes pia jana alicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya West Brom baada ya kutangaza kustaafu kucheza soka. Katika picha hii Scholes alikuwa anaingia uwanjani kucheza mechi yake ya 498 ambayo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwa Man utd
Handball: Spurs players react after referee Andre marriner fails to give a penalty
Jumapili ya jana tulishuhudia pia Tottenham wakitolewa nje ya nne bora na kupoteza nafasi yao ya ushiriki katika michuano ya UEFA champions licha ya kushinda kwa goli 1-0 dhidi ya Sunderland. 
Tribute: Stiliyan Petrov salutes the fans with manager Paul Lambert (left) after Aston Villa drew with Wigan
Stiliyan Petrov (kulia) jana pia aliwaaga mashabiki wa Aston Villa baada kugundulika na kansa na kuamua kustaafu soka.
Grand exit: Jamie Carragher has been a truly outstanding servant for Liverpool
Jamie Carragher pia alipigiwa makofi kama ishara ya kumshukuru na kumuaga katika mchezo wake wa mwisho baada ya kuamua kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 35.
Jump for joy: Fernando Torres celebrates scoring the winner for Chelsea and clinching them third spot
Torres akishangilia goli la ushindi ambalo limeiwezesha Chelsea kufikisha pointi 75, pointi ambazo zimeiwezesha Chelsea kuingia moja kwa moja kwenye michuano ya klabu bingwa ulaya (UEFA) 

No comments:

Post a Comment