Monday, May 20, 2013

Mashindano ya Zanaqua Cup yafunguliwa Zanzibar

Michuano ya Zanaqua cup imefunguliwa wikiendi hii na Mheshimiwa Abdilahi Jihad Hassan (waziri wa Mifugo na Uvuvi Zanzibar) ambaye alishawahi kuwa waziri wa michezo. Michuano hii inayozaminiwa na Zanaqua maji safi ya kunywa ni maalumu kwa ajili ya kuwakutanisha watu wanatoka kwenye makundi mbalimbali ya kijamii ambayo yametengwa (yatima, viziwi nk) dhidi ya waandishi wa habari, wasanii na wanafunzi ili kudumisha upendo na umoja baina ya makundi haya ya watu ndani ya jamii. Katika mechi ya ufunguzi iliyofanyika jumapili ya tarehe 19/5, timu ya wasanii wa bongo fleva iliweza kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi), michuoano hii itaendelea tena kwa kuwakutanisha waandishi wa habari dhidi ya vijana yatima. Mshindi katika michuano hii anatarajiwa kuibuka na kikombe cha Zanaqua na zawadi zingine mbalimbali ikiwemo fedha taslimu.   

Waliovaa jezi za bluu ni wasanii wa bongo fleva Zanzibar na jezi nyeupe ni wachezaji wenye ulemavu wa kusikia (viziwi)

Mgeni rasmi Mh Hassan (waziri wa mifugo na uvuvi Zanzibar) wa pili kushoto akielekea kuzikagua timu sambamba na mdau wa Michezoupdates Bw. Ilumbo Malaki wa kwanza kushoto mwenye suti nyeusi. 

Mh. Hassan pamoja na mdau wa MichezoUpdates Bw Ilumbo Malaki wakipata picha ya pamoja na timu ya watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) 









No comments:

Post a Comment