Tuesday, May 28, 2013

Nitamlipa zaidi Ronaldo - Rais wa Madrid

Bumper deal: Perez is prepared to break the bank to keep Ronaldo at Real

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amesema atahakikisha anamfanya Cristiano Ronaldo kuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi duniani ili asipate tamaa ya kuondoka Real Madrid. Perez aliyasema hayo kufuatia tetesi zilizopo kuwa Ronaldo anaweza kuhamia Man utd, PSG au Chelsea kutokana na kile kilichoelezwa kuwa na mahusiano mabaya na uongozi wa klabu hiyo. Perez alisema “nitafanya kila liwezekanalo nimfanye Ronaldo kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ya wote ili awe na furaha na asipate tamaa ya kuhama na tutahakikisha aondoki kwasababu ni mchezaji mzuri”.Nia hii ya raisi wa Madrid ikifanikiwa basi Ronaldo atazidi kupaa zaidi kimalipo duniani kwani hadi sasa yeye ndiye anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa kuliko wote duniani. Ronaldo analipwa dola mil 20.5 kwa mwezi, Messi dola mil 20, Rooney dola mil 17.8 na Kaka ni dola mil 14.3 (takwimu hizi ni kwa niaba ya Forbes). 

No comments:

Post a Comment