Tuesday, May 28, 2013

Carvalho asajiliwa na Monaco

Carvalho leaves Madrid for Monaco
Ricardo Carvalho amejiunga na klabu ya Monaco ya Ufaransa akitokea Real Madrid baada ya kumaliza mkataba wake. Carvalho amefikia uamuzi wa kuhama Madrid kutokana na ukweli kwamba nafasi yake ndani ya timu hiyo imekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Varane, Ramos na Pepe jambo ambalo limemfanya akae benchi karibia msimu mzima mara baada ya kupona majeraha yake. Carvalho mwenye miaka 35 amejiunga na Monaco kwa mkataba wa mwaka mmoja anategemea kusaini mkataba mwingine msimu ujao kama kiwango chake kitakuwa kizuri. 

No comments:

Post a Comment