Wednesday, June 26, 2013

Yanga kutoshiriki kupokea zawadi za ubingwa

Bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga leo imetangaza kutoshiriki kwenye utoaji wa zawadi za washindi wa ligi hiyo zinazotarajiwa kutolewa tarehe 3 Julai mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa Habari, msemaji wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema 'Yanga hatutoshiriki kwenye hafla hiyo kutokana na kuchelewa kutolewa zawadi hizo, ilitakiwa siku ile ile tunapokea kombe tupewe fedha zetu, lakini hadi leo hii wachezaji wanadai fedha zao tumeshindwa kuwapa kwasababu bado hatujapewa, jambo ambalo sio jema kwa maendeleo ya klabu'. Vodacom walipoulizwa kuhusiana na taarifa hizi, wamesema wamezipata kwa barua, ila kutokana na sababu mbalimbali ndiyo maana zawadi hizo zilichelewa kutolewa, lakini Vodacom imeuomba uongozi wa klabu ya Yanga kushiriki kwenye halfa hiyo bila kukosa ili kufanikisha zoezi hilo. Klabu ya Yanga inatarajia kukabidhiwa kiasi cha takribani mil 75 kama mabingwa wa ligi hiyo.   

No comments:

Post a Comment