Thursday, May 23, 2013

Stars yashiriki chakula cha mchana na Rais Kikwete

Timu ya taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars leo ilishiriki chakula cha mchana ikulu na Rais Dr. Kikwete ikiwa ni moja ya jitihada za serikali za kuipa motisha timu hiyo katika kuelekea kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Morocco. Katika hotuba yake Mh. Rais amesema "Taifa stars mnatakiwa kuwapatia raha Watanzania, nyinyi fanyeni kazi serikali ipo nyuma yenu, lazima tuwashangaze kwa kuwa wa kwanza kwenye kundi, sisi tutafanya kila linalowezekana nyinyi mshinde, hivyo na nyinyi lazima mjitume, hivyo, tunawatakia ushindi kwenye mchezo wenu ujao". Naye kocha wa taifa stars Kim na nahodha Juma Kaseja kwa pamoja wamewaahidi Watanzania ushindi na watajitahidi kwa uwezo wao wote kuiwezesha Stars kufuzu kwenye michuano hii. Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio hilo.      

Picha na 6Picha na 4Picha no 3

No comments:

Post a Comment