Thursday, May 23, 2013

Kocha wa Mali ajiunga na TP Mazembe

Kocha wa timu ya taifa ya Mali, Patrice Carteron ameipiga chini timu hiyo na kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Carteron amejiunga na klabu hiyo baada ya alikuwa kocha wa Mazembe Lamine N’Diaye kujiuzulu. Carteron amefunga mkataba wa miaka miwili na TP Mazembe licha ya kuwa kocha huyo atajiunga rasmi na Mazembe baada ya kumaliza mechi mbili za mwisho za Mali dhidi ya Rwanda na Benin za kuwania kushiriki kombe la dunia zinazotarajiwa kufanyika Juni 9 na 16 mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment