Friday, May 24, 2013

Timu 14 zitakazoshiriki ligi kuu Tanzania bara msimu ujao 2013/2014

Timu 14 ndizo zitakazoshiriki ligi kuu Tanzania bara msimu ujao, timu hizo ni Ashanti United, Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Oljoro JKT, Rhino Rangers, Ruvu Shooting, Simba, Tanzania Prisons na Yanga. Timu tatu kati ya hizi ndizo zilizopanda daraja ambazo ni Ashanti, Mbeya city na Rhino Rangers. Wakati huo huo shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya usajili kwa njia ya mtandao (Transfer Matching System-TMS) kwa klabu za Ligi kuu ya Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2013/2014. Semina hiyo inatarajiwa kufanyika jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF saa 3 kamili asubuhi ikishirikisha watu wawili kutoka kila klabu ambao ni TMS Manager, na ofisa mwingine wa klabu.

No comments:

Post a Comment