Friday, May 10, 2013

Vodacom yatangaza zawadi za ligi kuu

Wadhamini wakuu wa ligi kuu Tanzania bara kampuni ya mawasiliano Vodacom leo imetangaza zawadi za washindi mbalimbali wa ligi hiyo. Akiongea mbele ya waandishi wa habari meneja uhusiano mambo ya nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema Vodacom itatumia jumla ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya zawadi tu za ligi kuu. Baadhi ya zawadi hizo ni, bingwa Yanga watapewa shilingi milioni 70, mshindi wa pili Azam watapewa shilingi mil 35 na mshindi wa tatu anayetarajiwa kuwa Simba atapewa shilingi mil 25. Mwalim alisema pia, mchezaji bora, mwamuzi bora na mfungaji bora wote watapewa mili tano wakati timu yenye nidhamu ya juu itapewa mil 15. Zawadi hizi zinatarajiwa kutolewa siku ya mwisho wa ligi kuu Tanzania bara ambapo karibia timu zote zimebakiza mchezo mmoja kwa kucheza michezo 25 isipokuwa timu chache ambazo zitacheza wiki hii mchezo wake wa 24. 

No comments:

Post a Comment