Sunday, June 30, 2013

Arsenal, Tottenham na Fio kupata jibu wiki ijayo

Decision time: David Villa could be on his way to White Hart Lane
Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa anatarajia kutoa jibu wiki ijayo la timu atakayohamia msimu ujao wa ligi.  Arsenal, Tottenham na Fiorentina ndiyo klabu ambazo zimetangaza hadi sasa kumuwania mchezaji huyu. Villa kwasasa yupo nchini Brazil na timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la mabara, na anatarajia kurudi nchini Hispania wiki ijayo na kufanya mazunguzo na wakala wake na kuchagua timu atakayohamia. Villa mwenyewe amesema yupo tayari kwenda klabu yoyote itakayokuwa tayari kulipa paundi mil 12 ambazo Barcelona inahitaji kama ada ya uhamisho. Lakini hadi sasa Tottenham ndiyo klabu iliyopo kwenye nafasi kubwa ya kumnasa Villa zaidi ya Arsenal ambayo jitihada zake kubwa zipo kwenye usajili wa Gonzalo Higuain  

No comments:

Post a Comment