Leo usiku kutakuwa na mechi nzuri ya kuangalia kati ya
France na Spain. Timu zote ni nzuri na zina wachezaji wanaocheza kwenye ligi
kubwa barani ulaya. Katika kundi “I” France anaongoza kwa kuwa na pointi 10
akifuatiwa na Spain pointi 8. Kwenye mchezo wa leo Spain wamekamia kushinda ili
kurudisha matumaini ya timu yao baada ya kulazimishwa droo na Finland ijumaa
iliyopita kwenye uwanja wa nyumbani. Utamu wa mechi ya leo ni kuona nani
anakwenda kilele kwenye kundi “I” vile vile Spain na France wote wanajua kucheza
mpira wa kuvutia, tutaona nani mbabe.Vikosi vya Spain na France vinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo
France: Lloris, Jallet, Varane, Sakho, Evra, Pogba, Matuidi, Cabaye,Valbuena, Benzema, Ribery
Spain: Valdes, Arbeloa, Pique,
Ramos, Monreal, Xavi, Busquets, Alonso, Pedro, Fabregas, Iniesta
No comments:
Post a Comment