Monday, June 24, 2013

Klabu ya Napoli imetoa siku 26 kwa Cavani

klabu ya Napoli ya Italia imetoa siku 26 kwa klabu yoyote inayotaka kumsajili mchezaji huyo iwe imefanya hivyo, zaidi ya hapo hataruhusiwa kuondoka. Taarifa hizi zimetolewa na raisi wa klabu hiyo Aurelio De Laurentiis akisema 'tunawatangazia wale wanaotaka kumsajili Cavani kuwa tarehe 20 Julai ndiyo siku ya mwisho, baada ya hapo tutaanza kujiandaa na msimu ujao hivyo hatutakubali aondoke tena'. Taarifa hizi zimetolewa kwa lengo la kuzishinikiza klabu za Chelsea, Man city na Madrid kufanya haraka kumsajili mchezo huyo, lakini hadi sasa muafaka haujafikiwa kati ya Napoli na klabu hizo kwa vile ada ya uhamisho ambayo Napoli wanahitaji ni kubwa kulinganisha na ubora wa mchezaji mwenyewe. Napoli wanahitaji kiasi cha paundi mil 54 ili kumuachia Cavani. 

No comments:

Post a Comment