Sunday, June 23, 2013

Kocha amwambia Thiago hana namba ya uhakika

Kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Thiago Alcantara ameendelea kulazimisha uongozi wa klabu yake kumuachia aende Man utd baada ya kocha wa Barcelona Tito Vilanova kumwambia hawezi kumhakikishia namba ya uhakika msimu ujao wa ligi. Taarifa hizi zimepatikana kutoka kwa Baba mzazi wa Thiago (Mazinho Alcantara), ambaye wiki hii alikubaliana na mawakala wa Man utd kuwa mtoto wake atajiunga na United. Akihojiwa kuhusu uamuzi wake wa kutaka Thiago ahamie United, Mazinho alisema 'Baada ya kumalizika kwa michuano ya Ulaya chini ya miaka 21, Thiago alikutana na kocha wake Vilanova ili kupata uhakika wa namba kweye kikosi cha kwanza, kocha hakumficha kitu chochote, alimwambia ukweli kuwa hawezi kumpa uhakika wa namba, hakusema sababu ni nini, lakini sisi tunafahamu kuwa Iniesta, Cesc, Xavi na sasa Neymar ndiyo sababu, wao wanamwambia mtoto wangu kuwa aendelee kubakia Barca ili aje kuwa mrithi wa kina Xavi na Iniesta, lakini muda wa Thiago ni huu na sio baadaye, lakini binafsi naamini tutafikia muafaka ili mambo haya yaishe'. Msimu uliopita Thiago alipewa nafasi ya kucheza mechi 15 tu za ligi kati ya 38, hali hii ndiyo inampa wasiwasi Thiago kwasababu anaamini ujio wa Neymar utamfanya apumzishwe zaidi ya msimu uliopita, kitu ambacho kinamfanya afikirie kuhama ili aweze kupata muda wa kucheza mechi nyingi zaidi na nakujiwekea mazingira mazuri ya kupata namba kweye kikosi cha timu ya taifa kitakacho kwenda nchini Brazil kwenye kombe la dunia. 

No comments:

Post a Comment