Saturday, June 22, 2013

Simba yamtema rasmi Juma Kaseja

Klabu ya Simba imetangaza rasmi kumtema golikipa wake wa siku nyingi Juma Kaseja baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka kumi (10). Kaseja ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa, alisajiliwa na Simba mwaka 2003 akitokea klabu ya Moro United na tokea ajiunge na Simba, Kaseja alikuwa ni mlinda mlango tegemezi licha kuichezea Yanga msimu mmoja mwaka 2009. Uongozi wa Simba umesema, Kaseja ametemwa Simba kwasababu mkataba wake umekwisha hivyo kwasasa ni mchezaji huru na anaweza kusajiliwa na timu yoyote. Simba imefikia uamuzi huu baada ya kumsajili golikipa mpya kutoka Mtibwa Sugar Andrew Ntala na kuifanya klabu ya Simba kuwa na makipa watatu Ntala, Abel Thaira na Abuu Magube. Mbali ya kutemwa na Simba, Kaseja bado ana jina kubwa la kumuwezesha kupata timu ya kucheza ligi kuu msimu ujao ili aendelee kupigania nafasi yake kwenye timu ya taifa. 

No comments:

Post a Comment