Sunday, June 2, 2013

Neymar aiponda timu ya taifa England

Mbrazil Neymar ameiponda timu ya taifa ya England kwa kusema kuwa haina nafasi ya kushinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Neymar ameyasema hayo alipokuwa akiongea na The Sun kuhusiana na mechi ya kirafiki kati ya Brazil na England. Nemar alisema “Nawaheshimu sana wachezaji wa timu ya England kwasababu wanamafanikio makubwa sana kwenye klabu zao, vilevile wanacheza vizuri sana wakiwa na klabu zao ila wanapocheza kwenye timu ya taifa hawachezi vizuri kwa kujituma, ndiyo maana siwahofii kabisa kwenye kombe la dunia. Kuna timu kama Ujerumani, Hispania, Italia, Uholanzi na Argentina, hizi ndizo nazifikiria zitaweza kutupa ushindani mkali lakini sio England”. Maneno hayo ya Neymar yataanza kuthibishwa leo kwa kupima viwango vya Brazil na England wakati timu hizo zitakapochez mechi ya kirafiki inayotarajiwa kuanza saa nne usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki. 

No comments:

Post a Comment