Sunday, June 2, 2013

Suarez aongeza joto la kuhama Liverpool

Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ameendelea kuonesha hasira zake kwa vyombo vya habari vya nchini Uingereza na zaidi ameiponda pia kauli ya waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameron aliyoitoa baada ya Suarez kumng’ata Ivanovic. Suarez alisema “kwanini David Cameron anasema mimi sio mfano mzuri kwa watoto, ana wasiwasi tu na raia wake, na mimi siwezi kuomba msamaha kwa Waingereza kwasababu nina hasira sana na vyombo vya habari vya nchini hiyo, waandishi wamekuwa wakinifuata sana, jambo dogo wanalifanya kubwa, kila mahali ninapokwenda wananifuata, hata nikienda kumchukua mtoto wangu shule wanakuja pia, hata sijui wanataka nini, imefikia muda nimeshachoka, nataka kubadilisha mazingira, maisha ya Uingereza siwezi tena”. Suarez ameyasema hayo alipokuwa anaongea na vyombo vya habari nchini kwao wakati Uruguay ikijiandaa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa Juni 5. Kitendo cha Suarez kumponda waziri mkuu wa Uingereza hazarani kimeongeza joto ndani ya klabu ya Liverpool la kufanikisha uhamisho wa Suarez haraka kwani Liverpool wanafahamu fika kuwa serikali ya Uingereza haitakubali tena Sureaz kuwepo ndani ya nchi hiyo baada ya kumkejeli waziri mkuu David Cameron hazarani. Suarez ameshathibitisha kuwa wakala wake ameshakubaliana na Real Madrid na anatarajia msimu ujao atakuwa nje ya Liverpool.  

No comments:

Post a Comment