Tuesday, June 4, 2013

Ronaldo hatosaini mkataba mwingine na Real Madrid

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangaza kuwa hatosaini tena mkataba mwingine na klabu yake baada ya mkataba anaoutumikia sasa kuisha. Mkataba wa sasa wa Ronaldo unakwisha mwaka 2015, ikiwa ni miaka mitano tokea mwaka 2009 alipohamia Madrid akitokea Man utd kwa paundi milioni 80. Ronaldo alitoa kauli hiyo mara mbili mfululizo alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari nchini Ureno na Hispania jambo ambalo lilimfanya raisi wa Real Madrid Florentino Perez kutolea maelezo jambo hili na kusema "Ronaldo anamaliza mkataba wake 2015, na sisi tunajua hana furaha kuwepo Madrid, kwasasa tunajaribu kumfanya awe na furaha kwa kumpatia anachotaka (kuongezewa mshahara), ila hatutakuwa tayari kumuachia amalize mkataba wake na kuondoka akiwa mchezaji huru, sisi tumemnunua kwa pesa nyingi sana, tunataka kumuuza kwa pesa nyingi pia, tutajitahidi kuongea naye, ila ikishindikana hatuna budi tutamuuza pia kwa bei ya juu". Kauli hizi mbili za Ronaldo na Perez zinatoa njia kwa klabu za Man utd, Chelsea na PSG ambazo zinamuhitaji Ronaldo kwa msimu ujao. Klabu hizi zilikuwa bado hazijatuma maombi rasmi kwa Real Madrid kwasababu Madrid walikuwa hawapo tayari kumuuza, ila taarifa zilipo ni kuwa Real Madrid watamuuza kwa bei ya juu inayolingana au zaidi ya waliomnunulia, ila jambo hili litawezekana kama Madrid watafanikiwa kumsajili Gareth Bale wa Tottenham.  
Daylight: Cristiano Ronaldo (right) chats with friends after emerging from Lisbon's Lust nightclub at 7am
Ronaldo akiwa na marafiki zake alfajiri ya jumatatu wiki hii nchini Ureno wakitokea club kula starehe 

No comments:

Post a Comment