Klabu ya Chelsea imeitolea nje Barcelona kumsajili David Luiz kwa paundi mil 30. Klabu ya Barcelona ilituma ofa hiyo juzi ili kumsajili Luiz lakini taarifa zinasema, kocha wa Chelsea, Jose Mourinho aligoma mchezaji huyo kuuzwa baada ya kuonesha kiwango kizuri kwenye kombe la mabara. Luiz alikuwa hayumo kwenye mipango ya Mourinho kabla ya kombe la mabara kuanza, lakini Mourinho ameonesha kumkubali Luiz baada ya michuano hiyo kuisha na imesemekana atabaki Chelsea kwa msimu ujao. Barcelona wanamuhitaji Luiz ili kuziba pengo la Puyol ambaye ni majeruhi.
Moja ya save muhimu aliyoifanya Luiz katika mechi ya fainali kati ya Brazil na Spain. Tukio hili ndiyo moja ya sababu iliyompandisha jina Luiz na kuonekana ni moja kati ya mabeki muhimu sana kwasasa.
|
Tuesday, July 9, 2013
Mourinho aitolea nje Barca kumsajili Luiz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment