Sunday, June 16, 2013

Sina mpango wa kuhama Chelsea - Juan Mata

Mata is a fan favourite in west London (©GettyImages)
Kiungo wa Chelsea Juan Mata amekanusha vikali tetesi zilizopo kuwa anataka kuihama Chelsea na kujiunga na timu nyingine. Mata aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na gazeti la Marca kufuatia tetesi zilizopo kuwa Mourinho hamtaki Mata, Torres na Luiz kwenye kikosi chake. Mata mwenyewe alisema ' hizo taarifa sio za kweli na ninapenda kuwajulisha watu kuwa mimi bado ni mchezaji wa Chelsea, labda Jose mwenyewe aniambie kuwa sifai kwenye kikosi chake, lakini hadi sasa sijapata taarifa zozote, na hapa nilipo mawazo yangu yote ni kukutana na Mourinho akiwa kama kocha wangu, ninahamu ya kufundishwa na Jose, kwani ni kocha mzuri na uwezo wake unajulikana'. Mata kwasasa yupo nchini Brazil na timu ya taifa ya Hispania katika michuano ya Confederation cup, baada ya michezo hiyo anatarajia kuwa na likizo fupi kabla hajajiunga na Chelsea kushiriki kwenye mechi za kirafiki kimataifa. 

No comments:

Post a Comment