Monday, August 19, 2013

'Sina haraka ya kuwachezesha Messi na Neymar'

Kocha wa klabu ya Barcelona Tata Martino amesema hana haraka ya kuwachezesha pamoja washambuliaji wake Messi na Neymar ili kuona uwezo wao wakiwa dimbani. Martino ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa baada ya mechi ya jana kuisha huku Barcelona ikiibuka na ushindi wa goli 7-0 dhidi ya Levante. Martino alisema 'najua washabiki wa Barcelona na wadau wa soka wanapenda kuwaona Messi na Neymar wakicheza pamoja, lakini mimi nimekuwa mchoyo wa furaha zao kwasababu ya masuala ya kiufundi. Neymar bado mgeni ndani ya klabu, anahitaji muda kuzoea mazingira, lakini Messi amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu, hivyo, wachezaji hawa wanahitaji mapumziko kidogo. Kwasababu hii ndiyo maana wote hawakucheza dakika 90 katika mchezo wa leo, ila napenda kuwaahidi wadau wasoka na mashabiki wa Barcelona kuwa utafika muda watawaona wachezaji hawa wakicheza dakika 90 pamoja'. Katika mechi ya jana Messi na Neymar walicheza pamoja kwa dakika saba tu za kipindi cha pili, ambapo Messi alitolewa akaingia Iniesta na Neymar aliingia kuchukua nafasi ya Alexis. 

No comments:

Post a Comment